Dkt.Jingu atoa rai hospitali ya Amana uboreshaji mfumo TEHAMA.

Na Moshi said, Dar es salaam

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. John Jingu ameishauri hospitali ya Amana kuboresha utoaji huduma kw wagonjwa Kwa kutumia mfumo wa TEHAMA Ili kuokoa muda na huduma kuwa Bora ikiwemo kuwaona madaktari.

Hayo amesema Jijini Dar es Salaam  baada ya kufanya ziara ya kukagua  huduma za afya na utekelezaji wa miradi katika Hospitali ya Rufaa Mkoa Amana ambapo amesema kazi inaendelea vizuri.

Aidha amesema kuwa utumiaji wa mifumo hiyo itasaidia kuokoa muda wa kukaa hosptali kusubiria huduma kwani watajua huduma wanapata mda gani baada ya kupangiwa   siku na muda wa kumuona daktari husika.

Amesema huduma hiyo pia itamwezesha mgonjwa kupatiwa matibabu jambao ambalo litasaidia na kurahisisha kuimarisha utoaji huduma kwa wagonjwa pamoja na kuepuka kupoteza muda.

“Mtu kokote aliko awe anatoka Dar es Salaam ama mkoani basi atalazimika kupiga simu au kutumia mifumo ya barua pepe na mingine itakayowekwa kuomba kufika hospitalini hapa kutibiwa bila kujali simu ni ya kisasa au kitochi mfumo huo utawafikia,” amesema Dkt. Jingu.

Wakati huohuo Dk. Kingu ameweza kuwakabidhi hati ya umiliki wa ardhi Hospitali hiyo yenye ukubwa wa hekari sita ambapo awali walikuwa wakiendesha shughuli za matibabu bila kuwa na hati miliki.

Kwa upande wake Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa Amana Dkt. Bryceson Kiwelu amesema kuwa agizo hilo la Katibu Mkuu wamelipokea kwa mikono miwili kwani walikuwa wanakabiliwa na changamoto wa msongamano wa wagonjwa na malamamiko mengi kutoka kwa wagonjwa kutokana na kila mmoja kutaka kutibiwa kwa wakati.

Amesema wanajipanga kuanza kutoa elimu kwa wananchi na wagonjwa kuhusiana na matumizi ya teknolojia hiyo ya kutumia mifumo hiyo kabla ya kuanza kwa kutumia rasmi ili kuondoa sintofahamu kwa wagonjwa.

Amesema mfumo wa Tehama ulianza mwaka 2012 kwa kuwahudumia wagonjwa kwa kupatiwa majibu na huduma zingine lakini bila kutumia kwa kufanya miada kufika hapo ambapo wanajipanga kuanza muda si mrefu kutokana na gizo hilo.

“Mfumo huo utatusaidia kwa kiwango kikubwa kwani kinachotokea sasa hivi wagonjwa wote wanafika kwa wakati mmoja na kila mmoja ana ona yeye muhimu kupatiwa huduma kuliko mwingine” amesema Dk. Kiwelu.

Amesema wastani wa kupokea wagonjwa hospitalini hapo ni wagonjwa 650 hadi 700 kwa siku ambapo idadi hiyo imepungua toka kutokea kwa janga la Covid-19  ambapo awali walikuwa wakipokea wagonjwa 1000 na zaidi kuja kupata matibabu hospitalini hapo.

Aidha ziara hiyo iliweza kutembelea miradi ya hospitali hiyo ikiwemo kuona mtambo mpya wa kuchomea taka ambao utakuwa mradi wa kuingiza mapato ya ndani ambapo wataweza kupokea taka toka katika hospitali zingine na wataweza kuwahudumia huduma hiyo kwa kuwachomea kwa Shilingi elfu tano kwa kilo moja.

Comments