Na Moshi said, Dsm - 21 Juni 2024
WAVUVI nchini wametakiwa kuacha kufanya uvuvi haramu ili kuweza kusaidia kuondokana na tatizo la kuharibika kwa samaki pindi wanapovuliwa.
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) Dkt. Ismael Kimirei,wakati akifungua mafunzo ya siku tano ya kuwajengea uwezo katika usalama,ubora na stadi za biashara na masoko kwa wajasilimali wa mazao ya viumbe hai,mafunzo hayo yamefadhiliwa na taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya uvuvi (ABIST) inayojihusisha kuwajengea uwezo wavuvi nchini.
Dkt Kimerei,amesema lengo ni kupunguza kuharibika kwa bidhaa zitokanazo na Uvuvi toka asilimia 40 mpaka 20.
“Tunawaomba wavuvi waache uvuvi haramu,kutupa taka baharini ili kuondokana na mazao yatokanayo na bahari kuharibika pindi mvuvi anapovua”Amesema Dkt Kimerei.
Katika hatua nyingine,Dkt Kimerei,amewataka wajasiliamali wa mazao ya Viumbe maji kuhakikisha wanaongeza thamani ili kuweza kupata masoko ndani nje ya nchi
Akizungumzia mafunzo hayo Mwenyekiti wa taasisi ya ABIST,Profesa Yunus Mgaya,amesema mafunzo haya ni ya siku tano ya kuwajengea uwezo wakukuza bidhaa zao.
“Lengo la mafunzo kuwajengea uwezo waweze kukuza biashara zao na kuongeza Ubora”Amesema .
Kwa upande wake Fatuma Katula ambaye ni mjasiliamali ameishukuru ABSTI kwa mafunzo hayo na kusema yatawasaidia kuongeza masoko.
Comments
Post a Comment