KUELEKEA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA TGNP MTANDAO YAWATAKA WANAHARAKATI KUFANYA HAYA.

Kuelekea siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia washiriki wa semina za Jinsia na Maendeleo (GDSS) wametakiwa kuzitumia siku hizo kama kielelezo kizuri cha kuleta mabadiliko katika maeneo wanayoishi.

Afisa Program ya Harakati na Ujenzi wa Nguvu za Pamoja wa TGNP Mtandao Bi. Anna Sangai akitoa ufafanuzi wa jambo mapema jana jijini Dar es salaam.


Na Vicent Macha Dar es salaam.

Hayo yameelezwa mapama jana na Afisa Program ya Harakati na Ujenzi wa Nguvu za Pamoja wa TGNP Mtandao Bi. Anna Sangai wakati wakati akitoa elimu kwa wanaharakati na wananchi kutoka kata mbalimbali za jiji la dar es salaam.

Amesema kuwa kampeni hiyo kwa mwaka huu wa 2020 kitaifa itaratibiwa na shirika lisilo la kiserikali linaloitwa Mkuki, na uzinduzi wa kampeni hiyo utafanyika siku ya jumatano novemba 25 katika ukumbi wa (JNCC) Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam.

Afisa huyo ameongeza kuwa Siku 16 za kupinga ukatili wa Kijinsia ni kampeni  ya Kimataifa  inayoongozwa na Kituo cha Kimataifa cha wanawake katika uongozi tangu mwaka 1991 na kuadhimishwa kila mwaka ifikapo novemba 25 hadi desemba 10.

Ameendelea kusema kuwa  chimbuko la 16 za kupinga unyanyasaji wa kijinsia na mauaji ya kinyama ya kina dada wa Mirabelle yaliyofanyika nchini Dominica mwaka 1960 na Mwaka 1991 Umoja wa Mataifa (UN) ulichagua Novemba 25 iwe siku ya Kimataifa ya Kupinga Ukatili wa Kijinsia ambapo kilele chake huadhimishwa Desemba 10 ya kila mwaka.

Ameendelea kusisitiza kuwa lengo la maadhimisho haya ni kutoa fursa kwa wanawake, wanaume,Vijana wa kike na kiume na wanaharakati wengine kukuza uelewa wa umma juu ya mchango wa wanawake katika maendeleo na kutafakari matokeo ya harakati za ukombozi wa mwanamke Kimapinduzi sambamba na kutafakari mafanikio hayo kwa miaka 20 ya tangu kuanzishwa kwa harakati hizo nchini.

 

Na mwisho amesema kuwa Siku hizi 16 hutoa mwanga wa uelewa kwa jamii kwa siku nyingine muhimu kama Novemba 29 ambapo ni siku ya Kimataifa ya watetezi wa haki za Wanawake , Desemba 1,Siku ya Ukimwi Duniani, Desemba 6 siku ya mauaji ya kikatili ya Montreal 1989 (wanawake 14 waliuawa na mtu aliyekuwa anawachukia wanawake) na Desemba 10 siku ya Haki za Binadamu Duniani.


Mwanaharakati wa jinsia Bi. Nanteka Maufi akichangia mada katika kuelekea siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia mapema jana jiji Dar es salaam.
Washiriki wakifuatilia semina kwa umakini. 
Mwanaharakati kutoka kituo cha Taarifa na Maarifa kata ya Majohe Bw. Joseph Safari akitoa ufafanuzi wa jambo katika semina za jinsia na maendeleo (GDSS).
Semina ikiendelea.

Comments