SHIRIKA LA AGRI THAMANI FOUNDATION KUTOA MSAADA WA TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI WA SEKONDARI NCHINI

Mkurugenzi wa Agri Thamani, Mh Neema Lugangira (MB) kushoto akiwa na taulo za kike ambazo amezinunua kupitia ufadhili wa Ubalozi wa China kwa ajili ya kutoa msaada huo kwa wanafunzi wa kike wa
sekondari sasa unaanza rasmi ikiwa ni mkakati wa kuhakikisha watoto wa kike
wanaondokana na changamoto za kukosa masomo wakati wa kipindi cha hedhi kulia ni Mama Simba ambaye ni muzaji wa taulo hizo

Mkurugenzi wa Agri Thamani, Mh Neema Lugangira (MB) kulia akikagua taulo hizo

Mkurugenzi wa Agri Thamani, Mh Neema Lugangira (MB) kulia akikagua taulo hizo

Sehemu ya taulo ambazo zimezinunuliwa na Mbunge Neema Lugangira kwa ajili ya wanafunzi
kupitia ufadhili wa Ubalozi wa China kwa ajili ya kutoa msaada huo kwa wanafunzi wa kike wa
sekondar

Sehemu ya taulo ambazo zimezinunuliwa na Mbunge Neema Lugangira kwa ajili ya wanafunzi wa kike shule za Sekondari  kupitia ufadhili wa Ubalozi wa China

 MPANGO wa Asasi ya Kiraia NGOs ya Agri Thamani Foundation kutoa msaada wa taulo za kike kwa wanafunzi wa kike wa sekondari kupitia ufadhili wa Ubalozi wa China kuanza rasmi ikiwa ni mkakati wa kuhakikisha watoto wa kike wanaondokana na changamoto za kukosa masomo wakati wa kipindi cha hedhi.

 Hatua hiyo inatokana na leo Mkurugenzi wa Agri Thamani, Mh Neema Lugangira (MB) kufika kwenye Kiwanda cha Kays Hygiene na kukutana Mkurugenzi  wa kiwanda hicho Mama Simba  kuangalia oda ya taulo za kike za mabinti 1,500 ilipofikia.  

 Alipoulizwa  kwanini amekuja na mradi huu na kwanini amenunua taulo za kike nchini,Mh Lugangira alisema kwamba ameamua kufanya hivyo ili kuweza kuwasaidia mabinti wa kike kuondokana na vikwazo mbalimbali ambavyo wanakumbana navyo wakiwa kwenye siku za hedhi.

 Alisema  Agri Thamani wanalengo la kuimarisha lishe kwa vijana balehe hususani wa kike na hii inajumuisha hedhi safi na salama ili kuwawezesha kutimiza majukumu yao mengine ikiwemo kusoma kwa juhudi kubwa.

“Nimejionea changamoto kubwa ambao watoto wa kike wa vijijini hupata kila wanapokuwa kwenye hedhi na jinsi inavyoathiri masomo yao kupitia mahudhirio hafifu kipindi cha siku hizo”Alisema Mkurugenzi huyo.

Aidha alisema ili kuimarisha ufaulu wa mtoto wa kike Agri Thamani imekuja na programu ya kumsaidia mtoto wa kike aliye sekondari na ambae ataingia kidato cha 4 mwakani 2021 na anatoka mazingira magumu kupata msaada wa taulo za kike kwa kipindi cha mwaka mzima. 

“Tunaamini hii itamsaidia binti huyu kutokosa shule hivyo kumuongezea nafasi ya kufaulu vizuri zaidi katika awamu hii ya kwanza tutafikia wanafunzi wa kike 1,500 kutoka Mikoa ya Dodoma, Tabora, Kigoma, Kagera, Geita, Tanga na Lindi. 

Kwa upande wa Mama Simba alipoulizwa alipokeaje wazo hili na kwanini ameamua kuunga mkono juhudi za Mh Neema Lugangira alisema wameamua kuunga mkono juhudi za Neema Lugangira kwa sababu ni binti ambaye alikaa na kufirikiria watoto wa kike wa vijijini wasiojiweza kupitia shule.

“ Sisi Kays Hygiene tunauzoefu wa karibia miaka 40 na ni nadra sana kukutana na binti mwenye kujitoa kwa jamii namna hii hivyo huu ni mfano wa kuigwa hivyo tunampongeza sana Mh Neema Lugangira na tunaamini atakwenda kuwa mtetezi mzuri wa hedhi salama bungeni”Alisema

Hata hivyo alisema amefarijika kufanya kazi na Neema na huu ni mwanzo huku akihaidi kuendelea kumuunga mkono kwa kuhakikisha wanampa bei nafuu ambayo hawezi kupata kokote pale ili punguzo la bei iwe pia ni mchango wetu katika kuendeleza juhudi zake.

Comments