Chama cha Tadea kimesifu msimamo wa Rais wa serikali Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Maapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi unaowataka mawaziri kushirikiana vya vyombo vya habari kwa kutoa taarifa sahihi za utekelezaji.
Pia Tadea kimewatak askari wa usalama barabarani kusimamia sheria za usalama kutokana na ongezeko na kukithiri ajali za barabarani.
Ushauri huo umetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa ADA Tadea Rashid Yusuf Mchenga aliyesema baadhi ya madereva huendesha vyombo vya moto bila kujali sheria.
Mchenga amesema ajali za barabarani zimekuwa jangs linalopoteza nguvu kazi kutokana na watu kuwa vilema na baadhi kupoteza maisha.
Amekitaja chanzo cha kuongozeka ajali ni madereva kuendesha vyombo wakiwa hawana leseni,kutojua , kutoheshimu alama na sheria za barabarani.
Amesema kutokana na kukithiri ajali za barabarano ni jukumu la vyombo vya habari kuandika na kutangaza habari aidha za uzembe na madereva kutoheshimu sheria.
Mchebga amesema vyombo vya habari viandike habari za ongezeko la ajali kutokana na madereva kupuuza sheria za barabarani na kutaka zitungwe mpya.
Kwa upande mwingine Tadea kimevishauri vyombo vya habari kuendelea kueimisha kwa kuandika habari za kuongezeka vitendo vya ubakaji na udhalishaji wanawake na watoto.
Juhudi za kumpata mkuu wa usalama barabarani zanzibar ili kutoa ufafanuzi na kutaja takwinu za ajali za bado zinaendelea.
Mchenga amesema madereva wa vyombo vya moto hupita upande wowote wa batabara bila kuhofia sheria.
Amesema ikiwa utamaduni wa kuwafumbia macho wavunja sheria utaendelea wananchi watazidi kupoteza maisha na kuwa vilema.
Comments
Post a Comment