TULILIA NA SPIDI YA RAIS MAGUFULI MIAKA MIWILI YA MWANZO-MAMA SAMIA

 

Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan,baada ya kuapishwa kwa Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa , Waziri wa Fedha pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika hafla iliyofanyika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma

Na.Alex Sonna,Dodoma

Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan amefunguka  kuwa kasi waliyonayo wao na wateule wengine ni matokeo ya spidi ya utendaji kazi aliyonayo Rais Dk John Magufuli katika kuwatumikia watanzania.

Mama Samia ameyasema hayo leo jijini Dodoma wakati wa hafla ya kumupiasha Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.Philip Mpango na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof.a Palamagamba Kabudi Ikulu Chamwino Dodoma amesema kuwa  mwanzoni mwa serikali ya awamu ya tano walikuwa wakilia kutokana na kushindwa kwenda na kasi ya Rais Dk Magufuli.

Amesema miaka miwili ya kwanza ya Rais Magufuli wateule wengi walikuwa wakilalamika na kulia kila siku kutokana na kuishindwa kasi ya Rais mwenyewe lakini mwaka wa tatu waliizoea kasi hiyo na hata sasa wao watakuwa ndio wanaowanyoosha wateule wapya kwani tayari washaizoea spidi ya Rais.

” Ukweli Mhe Rais miaka miwili ya mwanzo tulikua tunalia na kukulaani sana, hatukua tumezoea hii kasi ambayo wewe mwenzetu unayo, siyo mimi, wala Waziri Mkuu na hao mawaziri wote tulikua tunalia na kulalamika, lakini leo hii wote tunasifu kazi yako na tunamuomba Mungu akulinde ili uendelee kutuongoza.

Ahadi yetu kwako ni moja, kama ambavyo umetuamini na ukaamua kurudi tena na sisi katika kipindi chako cha pili basi tutaendelea kufanya kazi kwa maslahi mapana ya Nchi yetu huku tukimtanguliza mbele Mwenyezi Mungu na kuwatumikia wananchi waliotuchagua,” Amesema Mama Samia.

Comments