Wanawake wametakiwa kuwa makini katika
mahusiano yao hususani wakati wa kutafuta mali na wapenzi wao ambao bado
hawajawaoa kwani hii uleta mkanganyiko hapo baadaye mwanaume anapofariki.
Hayo yameelezwa mapema jana na Naibu
Msajili wa Mahakama kuu ya Tanzania Bi. Devotha Kamazora alipokuwa akitoa elimu
ya namna ya kuandika wosia na faida zake katika Semina za Jinsia na Maendeleo (GDSS).
Naibu msajili huyo ameeleza kuwa
wanawake wengi wamekuwa wakijitoa sana kwa kuchukua mikopo na kufanya bishara
ndogo ndogo ili waweze kujenga pamoja na wapenzi wao na hali hawajaoana wala
kutambulisha kwa wazazi wao, hii huleta shida pale mume anapofariki au mume
anapoamua kuoa mke mwingine kwani hati na nyaraka zote unakuta anazo mwanaume.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia semina |
Ameongeza kuwa wengine unakuta anajua kuwa ni mume wa mtu nae kwa mapenzi anakubali kuwa nyumba ndogo na baadae akiachwa anajikuta hana kielelezo chochote kama risiti za kununulia vifaa hata fundi hamjui hivyo inakuwa ngumu mahakamani kumpa haki na mwisho kusababisha kupoteza haki yake ya msingi.
Ameendelea kusema kuwa kuandika wosia
si kama wengi wanavyodhani kuwa ni uchuro kwani wosia ni muhimu ili kuepusha
migongano ndani ya familia hasa mzazi mmoja napofariki hasa baba.
Aidha ameongeza kuwa cha msingi ni
kwamba mtunza wosia aweni mtu mwaminifu ili baadae sije kuleta shida baada ya
muhusika kutokuwepo huku akisisitiza mahara sahihi pa kuhifadhi wosia huo ni
mahakamani, kanisani hata kwa watu unaoweza kuwaamini kuwa hataleta shida
baadae.
Baadhi ya wakazi wa Dar es salaam wakifuatilia semina ya umuhimu wa kuandika wosia.
Naibu msajili huyo ameendelea kusema kuwa mzazi anaweza
kutoa mali yake yote kwa taasisi kama msikiti au kanisa hata kwa watoto yatima
lakini ahakikishe kuwa watoto wake amewapatia urithi wao na kama hataki kufanya
hivyo ni lazima atoe sababu za kutofanya hivyo, na sababu moja wapo kubwa ni
kwamba mtoto wako akitembea na mama yake au wakike na baba yake unaruhusiwa
kumtoa kwenye urithi na mahakama inakubali hoja hiyo.
Ameendelea kusisitiza kuwa mahakama inatambua
sheria ya kiislamu hivyo ukiandika wosia wako kuwa mgawanyo ufanyike kwa sheria
ya dini ya kiislamu basi mahakama itafanya hivyo kwa kugawa kulingana na dini
hiyo, lakini pia sheria aimpi mamlaka mrithi wa kiume kuuza mali iliyoachwa na
wazazi wake.
Na mwisho amewasisitiza wanaume kote nchini kuwa
na utaratibu wa kuandika wosia kwani inasaidia kupunguza migongano ndani ya
familia, na ameendelea kusisitiza kuwa wosia unaweza kubadilika kutokana na
matakwa yako mwenyewe kwa kubadilisha mashahidi au kugawa upya mali lakini
unachotakiwa ni kufuta usia uliyopita kwa kukanusha katika huu mpya.
Semina ikiendelea.
Comments
Post a Comment