Muwezeshaji wa semina Jackson Malangalila akitoa ufafanuzi wa jambo mapema leo jijini Dar es salaam katika semina za GDSS. |
Katika kuboresha na kuimarisha semina za Jinsia na Maendeleo (GDSS) washiriki wa semina
hizo wamepata nafasi ya kutoa maoni yao nini wanakihitaji kiongezeke au kipungue ili kuboresha semina hizo kwa mwaka 2021.
Fursa hiyo imetolewa
mapema leo jijini Dar es salaam na Afisa wa Dawati la Habari na Mawasiliano wa TGNP Mtandao Jackson Malangalila
wakati wa kufunga semina hizo kwa mwaka 2020 na kujiandaa na mwaka mwingine wa
2021.
Akikusanya maoni
ya washiriki wa semina hizo leo Disemba 16, 2020 Malangalila amewataka
washiriki hao kuweza kufanya kazi kama timu ili kuhakikisha GDSS ya mwaka unaokuja
inakuwa moto, Na kuweza kuongezeka kwa idadi ya washiriki ili elimu
inayotolewa iweze kuifikia sehemu kubwa ya jamii.
Baadhi ya
washiriki katika kutoa maoni yao walihitaji GDSS ijayo itakayoanza january 2021
kuwe na ratiba ya masomo ya mwaka mzima yatakayofundishwa, ili kila mtu awe
anajua siku gani kutakuwa na kitu gani na hata kwa wale walimu wahusika waweze
kujiandaa mapema kwa kujua siku watakazo hitajika kufundisha na watahitajika wafundishe nini.
Lakini pia
wadau wameomba kuwe na chumba maalum kwa ajili ya watu wa GDSS ili kuweza
kutunza vitu vyao kama wana GDSS, mfano watu wa sanaa za maigizo, ngoma nk. waweze kutunza zana za pamoja
na kuwa na uhifadhi wa kazi zote za wana GDSS ili kila kitu kinachowahusu
kiweze kuwepo humo ndani.
Wameendelea kusema
kuwa TGNP Mtandao iendelee kuwashika mkono wanaharakati wadogo wanaochipukia wanapojaribu
kuibua kesi mbalimbali ili wasivunjike moyo wakati wa ufuatiliaji na hatimaye waweze kufikia ndoto zao za kuwa wanaharakati wakubwa, kwa kuwa inafahamika
wanaharakati wengi wakubwa wanatokea katika jukwaa hilo la GDSS.
Aidha wanaharakati hao wameitaka TGNP kuendelea kuenzi kazi zinazofanywa na wana GDSS katika kupambana na ukatili wa kijinsia kwa kuchukua stori zao na kuziweka kwenye makablasha TGNP, ikiwezekana yawekwe maktaba ili hata wageni wakija waweze kuona kazi zinazofanywa na jukwaa hilo.
Lakini pia kuthamini mchango wa wana GDSS kwa kuwapa zawadi mbalimbali kama tuzo, vyeti nk. kwa wale wanaofanya vizuri katika kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia ili kuwapa motisha na wengine na wao wafanye kazi kwa kujituma kama wenzao waliopata tuzo.
Mwanaharakati wa ngazi ya jamii Kenedy Macher akitoa ufafanuzi wa jambo mapema leo jijini Dar es salaam.
Semina ikiendelea. |
Mwanaharakati kutoka Mbezi Hance Obote akiongea na wanaharakati wenzake juu ya mipango mipya ya GDSS ya mwaka 2021. |
Semina ikiendelea. |
Comments
Post a Comment