Vicent Macha Dar es salaam
Mh. Batuli amesema kuwa Chuchu Dote amekuwa mfano wa kuigwa na jamii kwani ameitekeleza sera serikali ya awamu ya tano kwa vitendo ya kuanziasha viwanda, Kwani amejipambanua kuwa mzalendo wa kweli kwa kumuunga mkono Rais John Pombe Magufuli.
Ameongeza kuwa vijana wengi waachane na dhima ya kusubiri kuajiliwa na matokeo yake wawekeze nguvu zao katika kujiajiri kama ilivyo kwa Chuchu Dote leo, Kwani amehitimu degree yake na kaamua kuachana na mambo ya kutafuta ajira na kuamua kujiajiri na kuweza kutoa ajira kwa vijana wenzake.
Aidha ameedelea kusisitiza kuwa bidhaa za Chuchu Dote ni nzuri kwani ni za asili na azichubui Ngozi bali zinaimarisha na kuifanya Ngozi yako iwe nzuri, pia amependa kuwasihi wakina mama pamoja na wakina baba kutumia bidha hizo kwani hazina kemikali zozote na zinafaa kwa watu wa aina zote
Kwa upande
wake mmiliki wa Dote Naturalz court Chuchu Dote amesema kuwa kwa Tanzania
atakuwa ni msanii wa kwanza wa vichekesho vya jukwani (stand up comedy) kuweza
kumiliki kiwanda kidogo na pia kuwa na mfanikio makubwa kama haya. |
Aidha amesema changamoto kubwa kwa Tanzania ni kwamba watu wakisikia vitu vya asili mawazo yao uja kwa watu weusi tu,
“Kwani mtu unapomwambia bidhaa hii ni asili anakwambia hivyo ni vitu vya watu weusi na siyo kwa sisi weupe na wanasahau kuwa unaweza kuwa mweupe na ukawa natural kwa kutopaka vitu vyenye kemikali, hiyo ndio shida kubwa kwa wateja wetu wengi”. Amesema Chuchu Dote
Bidhaa zinazotengenezwa na Dote Naturalz ni mafuta ya nywele, mafuta ya ngozi (lotion), shampuu za nywele na sabuni. Na vyote ni vya asili vinatengenezwa na vitu vya asili kama maji ya madafu, nazi, parachichi n.k
Ameendelea kuwasisitiza watanzania wote kutumia bidhaa za Chuchu Dote kwani zinasaidia kufanya Ngozi iwe nyororo na nadhifu pamoja na mafuta ya dote yanasaidia kukuza nywele na kuzipa muonekano mzuri.
Na mwisho amewataka vijana kujituma ili kuweza kufikia mafanikio wanayoyataka lakini pia kujikita katika ubunifu ili kuimarisha uchumi wa nchi yetu na kumsaidia Rais wetu katika kukuza na kuinua sekata ya viwanda.
Wageni wakifuatilia shughuli ya uindui wa Dote Natural Court. |
Mkurugenzi wa Dote Naturalz Court, Chuchu Dote Masaburi akionesha baadhi ya bidhaa zinzotengenezwa katika kiwanda chake kilichopo Mikocheni na Tabata jijini Dar es salaam. |
Mkurugenzi Mtendaji na mmiliki wa wa Dote Naturalz Court Chuchu Dote Masaburi akielezea baadhi ya bidhaa zinazopatika katika kiwanda chake mapema jana jijini Dar es salaam. |
Mkurugenzi wa Dote Naturalz akiwa katika picha ya pamoja na wageni waalikwa waliofika katika shughuli hiyo ya uzinduzi Dote Naturalz Court |
Baadhi ya bidhaa zinazopatikana Dote Naturalz Court |
Muonekano wa logo ya dote natural court |
Comments
Post a Comment