Sheikh Jalala amewataka watanzania kuendelea kumuenzi Hayati JPM, kwa Uzalendo wake kwa taifa la Tanzania.



Kiongozi wa Waislamu Madhehebu ya Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala amemsifu aliyekuwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli kwa ujasiri wake mkubwa na wa wazi wa kumbambana dhidi ya Mabeberu ambao walikokuwa wanainyonya nchi yetu.

“Hayati Dkt John Magufuli alitueleza jambo kumbwa mno na jambo muhimu kuwa kutambua na kutueleza mbinu za mabeberu, mbinu za wanyonya damu, watu wanaotaka siku zote wa ishi kwa migongo ya wa Tanzania na migongo ya wa Afrika.Kwa kweli kwa tendo lake la kuuzungumza ubeberu na kuwazungumza wanyonya damu, na kwamba lau si wanyonya damu, wa Afrika tusinge ishi katika mazingira ya umasikini na hali tuliyonayo na wala tusinge kuwa na maradhi haya tuliyo nayo yanayotumaliza kila siku” alisema Kiongozi Sheikh Jalala

Kiongozi Sheikh Jalala alisema hayo jana, katika Khutba Swala ya Ijumaa, Masjid Ghadir, Kigogo Post Dar es Salaam na kusema kuwa Hayati Dkt John Magufuli atakunbukwa kwa jambo lake la kumtanguliza Mungu kwa kila jambo na kila hali.

“Hayati Dkt John Magufuli alimtanguliza Mungu katika mambo yake yote, katika hotuba zake, katika mikutano yake, awe amekaa awe amesimama, kwa kweli Mungu alimtanguliza mbele. Bali wakati mwingine huwenda Viongozi wa Dini walirudi nyuma, yeye alikuwa mstari wa mbele katika kumuamini Mungu”. Alisema Kiongozi Sheikh Jalala.

Aidha Kiongozi Sheikh Jalala amesema kuwa Hayat Dkt John Magufuli hatosahauliwa katika Nyanja ya kudumisha na kuenzi Amani, Upendo, mshikamano na Umoja na kuwataka Watanzania wasikubali kuhatarisha Amani, mshikamano na umoja.

Hayati Dkt. John Pombe Magufuli enzi za uhai wake.

“Hayati Dkt John Magufuli alikuwa mpenda Amani, mpenda umoja, mpenda mshikamano ambayo ndio misingi mikubwa ya Taifa letu la Tanzania. Taifa la Tanzania litapigiwa mifano, na wenzetu wanaona gere, utulivu tulionao, Amani tulionayo na mshikamano tulionao” Alisema Kiongozi Sheikh Jalala.

“Niwaombe Watanzania kwenye kipindi hiki ambacho ni cha majonzi, ni kipindi cha huzuni, ni kipindi cha kutafakari, tuzidi kudumisha Umoja, mshikamano wetu, tuzidi kuenzi Amani ya nchi yetu na tusiyakubali maneno ya mtu yeyote yanayoandikwa iwe katika facebook, iwe ni twitter, iwe ni Instagram, iwe ni mahala gani, ambapo maneno hayo yatajaribu kuwatikisa Watanzania na kuwatoa katika mstari wao wa umoja, amani na mshikamano, Poleni sana Watanzania, Pole sana Mama yetu Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu” Alisema Kiongozi Sheikh Jalala.

Comments