Ujumbe wa Waziri Masauni kwa Askari Polisi wanaoshiriki mbio za SARPCCO GAMES

 

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amewataka askari Polisi wanaoshiriki michezo ya Shirikisho la Jumuiya ya Majeshi ya Polisi ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SARPCCO GAMES) kuzingatia taratibu zote na kanuni za michezo ikiwemo kujiepusha na vitendo ambavyo havikubaliki kimichezo.

Waziri Masauni amesema hayo wakati akifungua rasmi michezo hiyo katika uwanja wa uhuru jijini Dar es salaam, leo Septemba 10, 2022, ambapo pia aliwataka askari kujiepusha na rushwa, kupanga matokeo ya kimichezo na kuwataka kujenga uhusiano utakao saidia kudhibiti uhalifu unaovuka mipaka, usafirishaji wa binadamu sambamba na uhalifu mwingine.

"Askari mnaoshiriki michezo hii ya Majeshi (SARPCCO) nawataka mujiepusha na rushwa, kupanga matokeo ya kimichezo na mjenge uhusiano utakao saidia kudhibiti uhalifu unaovuka mipaka, usafirishaji wa binadamu sambamba na uhalifu mwingine,"

Kwa upande wake Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Camilius Wambura amesema kuwa, takribani nchi nane zinazoshiriki mashindano hayo ambayo yanawakutanisha askari na maofisa kwa pamoja na kuweza kuwa karibu na kufahamiana, na kufanya kazi kwa pamoja na kubadilishana taarifa mbalimbali za uhalifu na kiintelijensia.

Comments