CHAMA cha Wakulima nchini (AAFP), kimemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuruhusu mikutano ya hadhara

CHAMA cha Wakulima nchini (AAFP), kimetangaza mpango wake wa kuanza kufanya mikutano ya hadhara kuanzia February 2023, baada ya kufanya mkutano wake mkuu kesho Jumapili, jijini Dar es Salaam.

Taarifa hiyo imetolewa Leo Jumamosi, tarehe 11 Februari 2023 na Mwenyekiti wa AAFP Taifa, Said Sudi Said, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, kwenye Uchaguzi wa Jukwaa la Wanawake na Vijana la chama hicho.
"Mikutano ya hadhara ni haki yetu, chama kinategemea kuanza mikutano lakini katika mazingira ya uadilifu sababu sio sehemu ya kufanya fujo, Bali ni sehemu ya kufanya maendeleo na kueleza ushauri wetu juu ya namna Gani ya kupata Yale tunayohitaji. Katika demokrasia huwezi sema kiongozi hafai sababu unayotaka hayatekelezwi unapaswa kuyaeleza ili yatekelezwe," amesema Said.

Said amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuruhusu mikutano ya hadhara, huku akiusifu uongozi kwamba umekuwa chachu Kwa wanawake nchini katika kufikia nafasi za juu za uongozi wa nchi.

Akizungumzia uchaguzi huo, Said amewataka wajumbe kuchagua viongozi imara watakaonisaidia chama hicho kupata matokeo mazuri katika chaguzi zijazo.
Naye Kaimu Makamu Mwenyekiti wa AAFP Taifa, Nancy Mrikaria, amewataka viongozi wa jukwaa la wanawake watakaochaguliwa wahakikishe wanakiinarisha chama ili kipate wanachama wengi zaidi.

Comments