Dar es salaam, 22 Machi 2023.
Na Moshi said.
KATIKA kuhakikisha wanaboresha sekta ya Afya nchini,Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Amana imeanza utoaji wa huduma ya kipimo CT-SCAN kwa wagonjwa wote wanaotaka huduma hiyo.
Hayo yamebainishwa leo Jijini Dar es Salaam na Mganga mfawidhi Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Amana,Dkt Bryceso Kiwelu,wakati wa akitambulisha mashine za kipimo hicho kwa waandishi wa habari.
Dkt Kiwelu amesema mashine hizo ambazo zenye thamani ya bilioni ya 1.8 zitasaidia katika uharakishaji wa kutoa huduma hospitalini hapo.
"Uwepo wa mashine hii itatusaidia sana kutoa huduma maana hapo mwanzo wagonjwa tulikuwa tunawapeleka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kupata kipimo cha CT-SCAN lakini sahivi huduma itapatikana hapa"Amesema Dkt Kiwelu.
Aidha,Dkt Kiwelu,amewataka wananchi kunaohitaji kipimo hicho kujitokeza hospitalini hapo kwa ajili ya kupata kipimo hicho hata wale wenye bima pia.
"Nampongeza serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa jitihada zake za kuinua huduma za afya na hatua yake kutupa fedha kwa ajili ya ujenzi wa jengo la CT-SCAN hospitalini hapa,tunawataka wananchi waje kupata huduma."Ameongeza kusema Dkt Kiwelu.
Mbali na huduma hiyo na kipimo hicho pia hospitali ya Amana imeanzisha pia kipimo cha X-ray mashine kwa ajili ya kusafisha damu kwenye figo ambapo inathamani ya milioni milioni 400.
Kwa upande wake mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Amani ,wilaya ilala,Daniel mpanduji,ameipongeza serikali ya Rais Samia kwa kutenga fedha hospitalini hapo .
"Tunampongeza sana Rais Samia kwa kutoa fedha ,tunaamini wananchi wangu watapata huduma,hapo mwanzo kulikuwa na changamoto hapa Hospitali ya Amana,ila baada ya Rais kutoa Fedha huduma imekuwa nzuri sana"Amesema Mpanduji.
Comments
Post a Comment