Dkt. Oliver aiomba serikali kuweza kurejesha Masomo ya Dini mashuleni

Nabii Dkt Oliver Edward Mwiga Kiongozi wa Huduma ya Nguvu ya Ufufuo wa Karama za roho Mtakatifu na Udhihilisho wa Moto (REPOHIM) akiongea na Waandishi wa habari Kanisani kwake Jijini Dar es salaam.

Kutokana na kukua kwa Wimbi la  Mmomonyoko wa Maadili kwa Jamii Masomo ya Dini yanatakiwa kuanza kufundishwa ili kusaidia Watoto kuanza kujifunza kumjua Mungu nakua na hofu ya Mungu katika Maisha yao nakuachana na Vitendo Viovu, Jamhuri Digital imeelezwa.

Hayo yameelezwa Jijini Dar es salaam Mei 5 2023  na Nabii Dkt Oliver Edward Mwiga ambaye ni Kiongozi wa Huduma ya Nguvu ya Ufufuo wa Karama za roho Mtakatifu na Udhihilisho wa Moto (REPOHIM) wakati akizungumza na Mwandishi wa habari kanisani hapo.

Dkt Oliver amesema kwamba kipindi cha nyuma kulikuwa na mfumo mzuri wa ufundishaji wa Masomo ya Dini ya kikristo na kiislamu kuanzia Shule za Msingi hadi elimu ya juu hatua ambayo ilisaidia kwa kiasi kikuwa vijana kukua katika maadili mema.

“Napenda kuishauri serikali ishirikiane na Viongozi wa Dini kurudisha mfumo wa kufundisha mafundisho ya dini mashuleni kwani mfumo huu ulisaidia sana vijana kuwa na Taifa lenye vijana wenye maadili mema,lakini kwa sasa tunasumbuliwa na utandawazi ambao unaharibu maadili ya  watoto wetu ndio maana baadhi yao wameanza kujiingiza katika matendo yasiyofaa kama vile Ushoga,Mapenzi ya Jinsia Moja  na Usagaji.’amesema

Nakuongeza kuwa “Watu waliojiingiza katika vitendo vya ushoga,Mapenzi ya Jinsia Moja ,usagaji na uraibu wa aina mbalimbali tusiwanyanyapae hivyo tunapaswa kuwaombea kwa Mungu waacha kabisa vitendo hivyo.

“Tuendelee kutoa elimu kwa jamii kupitia njia mbalimbali kama vile vipeperushi,Kampeni za kitaifa na mijadala mbalimbali kuelezea jamii madhara yatokanayo na tabia za Usagaji,Ushoga na Mapenzi ya jinsia Moja ambayo yamekuwa yakipigiwa upatu na baadhi ya mataifa ya magharibi”amesisitiza Dkt Oliver

Aidha amendelea kuwakumbusha Wazazi kukaa karibu na Watoto wao ili kujua changamoto  zinazowakumba nakuweza kuchukua hatua haraka kabla madhara hayajajitokeza kwa watoto wao.

“Wazazi tuwajibike ipasavyo katika malezi ya watoto wetu licha ya kua bize na kazi za kutafuta kipato lakini kutenga muda wa kukaa na watoto wetu ni jambo la msingi sana”amesema Dkt Oliver

Comments