Ahmadiyya Muslim Jamaat Tanzania Yaandaa Mkutano Mkubwa, Mgeni Rasmi Makamu wa Rais Dkt. Mpango

 Na MOSHI SAID

Makamu wa Rais Dkt Philip Mpango anatarajiwa kuwa mgeni wa heshima  katika Mkutano Mkuu wa 52 wa jumuiya ya Waislamu Waahmadiyya Tanzania " JALSA SALANA" utakaofanyika Septemba 29 hadi Oktoba 1 ,2023 Kata ya Msongola Manispaa ya Ilala Mkoani Dar es salaam.

Hayo yamesemwa Mapema leo Septemba 28 ,2023 jijini Dar es salaam  na Naibu AMir ( Deputy Head) Abdulrahman Mohammed Ame kwa niaba ya Amir and Missionary Inharge Ahmadiyya Muslim Jamaat  Tanzania wakati akizungumza na Waandishi wa habari kuelekea Mkutano huo.

Amesema kwamba  kupitia Mkutano huo waumini watapata nafasi ya kusikiliza hotuba na nasaha za wataalamu wa Jumuyiya ambapo miongoni mwa mambo yatakayozungumzwa ni namna bora ya kuwalea watoto ikiwemo kujali elimu yao ya dini na sekula yaani kujitahidi kuwa raia wema kwa kuishi kwa amani na watu wote na kuwa watiifu kwa sheria za nchi.

 Naibu Amir Abdulrahman ameendelea kusema kuwa katika Mkutano huo waumini watakumbushwa juu ya umuhimu wa kujiepusha kuchanganya dini na siasa kwani jambo hilo huleta mkanganyiko na kuzalisha mianya ya ama wanasiasa kuitumia dini vibaya au watu wa dini kuitumia siasa vibaya kwa ajili ya maslahi yao binafsi.

 Aidha amesema kuwa kauli mbiyu ya Jalsa ya Mwaka huu hapa nchini ni " Tawheed ya kweli haiwezi kusimamishwa na bila ya Ukhalifa" ikiwa na maana ya kuwa mfumo wa Ukhalifa ulioanzishwa na Mwenyezi Mungu tangu zama za Nabii Adam ndio njia pekee ambayo Mwenyezi Mungu hudhihirisha Umoja wake hapa duniani na leo hii Tawheed ya kweli itasimamishwa kupitia Ukhalifa ulioanzishwa tena na Mwenyezi Mungu katika Uislam sawa na ahadi iliyotolewa na Mtume Muhammad s.aw.

 Aidha amesema kuwa Jumuiya ya Waislam Waahmadiyya ni Jumuiya ya Kimataifa inayopatikana kwenye zaidi ya nchi 212 duniani ikiwa nchini ya Kiongozi mmoja( Khalifa Mtukufu) 

 " Lengo lake kuu ni kutangaza kwa amani ujumbe sahihi wa Islam duniani kote na kuwa mstari wa mbele katika kupinga maana zisizo sahihi zinazonasibishwa na mafundisho ya uislam kama vile dhana potofu za ugaidi na misimamo mikali isiyovumilia wengine" amesema Naib Amir Ahmadiyya Muslim Jamaat Tanzania Abdulrahman 

Nakuongeza kuwa katika mkutano huo viongozi wa kitaifa wa serikali,vyama vya siasa ,viongozi wa dini mbalimbali na jamii kwa ujumla watashiriki katika kutoa nasaha zao nakwamba idadi ya washiriki inakadiriwa kuwa 5000 hadi 6000 kutoka maeneo mbalimbali nchini wanatarajiwa kuhudhuria Jalsa hii ya 52 na pia washiriki kutoka nchi za Kenya,Uganda na Ghana wanatarajiwa kuhudhuri

Awali akisoma ujumbe wa Kiongozi Mkuu wa Ahmadiyya Duniani Amir  & Missionary  Inharge wa Ahmadiyya Muislim Jamaat Tanzania Tahir Mahmood Chaudhry amesema kwamba Mkusanyiko huo umejengwa juu ya uungwaji mkono kamili wa ukweli na uenezaji wa uislam ambapo jiwe la msingi la jumuuiya hiyo limewekwa na mwenyezi Mungu.

" Nimuhimu kwamba mnufaike kikamilifu na mwenendo ya Jalsa hii ili kujifunza jinsi ya kuboresha viwango vyenu vya kiroho na kimaadili , kuwa bora katika kufanya vitendo vya ucha Mungu ni hivyo kupata ukaribu kwa mwenyezi Mungu Mtukufu " imesema taarifa hiyo.

Aidha taarifa hiyo pia imeongeza Washiriki wa Jalsa hiyo wanapaswa kuzingatia wajibu wao kuhusu mahubiri ambayo ni muhimu kwa kila ahmadiyya kupanga nakubuni njia mpya na zenye hekima kueneza ujumbe wa amani wa Islam ahmadiyya kote Tanzania na nchi jirani.

Naye Amir Ahmadiyya Muslim kutoka nchini Ghana Mohammed Bin Salih amesema kwamba amefurahishwa kupewa mualiko wa kuja kushiriki Jalsa hapa nchini huku akisema kuwa mkusanyiko huo unasaidia vijana kubadilika kimalezi na kiimani amewasisitiza Watanzania kujitokeza kushirikia Mkusanyiko huo.-

Comments