Tunzaa Digital Holdings Limited na Kampuni ya Simu ya Mkononi ya Vodacom kupitia M-pesa zimetangaza ushirikiano Mkubwa wa kibiashara
Kampuni ya Tunzaa Digital Holdings Limited na Kampuni ya Simu ya Mkononi ya Vodacom kupitia M-pesa zimetangaza ushirikiano Mkubwa wa kibiashara ambapo Wateja wa Vodacom watatumia aplikesheni ya Tunzaa ndani ya aplikesheni ya M- pesa kuweza kununua bidhaa mbalimbali.
Akizungumza wakati wa kutangaza ushirikiano huo jijini Dar es salaam Mkuu wa Kitengo cha Wateja TUNZAA Abdallah Said amesema kwamba kwa sasa watumiaji wa Tunzaa wanalipia kidogokidogo yaani" Tunza sasa ,Nunua baadae",yaani kwa kudunduliza kwa kipindi cha hadi miezi sita kwa bidhaa yoyote atakayoichagua.
Abdallah amesema hivi sasa Watumiaji wa Tunzaa wanaweza kununua bidhaa mbalimbali kwa kudunduliza zikiwemo vifaa vya nyumbani,runinga,mashine za kufulia ,majokofu ,simu za mkononi na vifaa vingine ambapo Tunzaa inapatikana kwa kupakua aplikesheni kupitia simu janja za mkononi za aidha Android ama iOS,au wanaweza kununua bidhaa kwa kutembelea tovuti ya Tunzaa ambayo ni www.tunzaa.co.tz
Mkuu huyo wa kitengo cha huduma kwa wateja Tunzaa pia amesema kwamba lengo la Tunzaa nikuimarisha tabia chanya za kifedha kwa Waafrika wa kila siku kwa kuwawezesha kununua bidhaa kwa njia ya awamu bila madeni kwa sasa Tunzaa inatoa huduma zake Tanzania nzima na hapo baadae ina lengo la kutanua wigo kufikia nchi za jirani kama Kenya,Uganda,Kongo,Zambia ,Malawi,Msumbiji,na baadae kufikia nchi zote za kiafrika.
" Tunzaa ina furaha kutangaza ushirikiano mkubwa na kampuni ya Vodacom kupitia aplikesheni ya M- pesa ,kuanzia leo wateja wote wa vodacom wanaotumia huduma ya M-pesa kwa ajili ya kufanya miamala yao wataweza kupata huduma ya kununua bidhaa mbalimbali kwa kulipa kidogo kidogo kutoka kwenye aplikesheni ya Tunzaa itakayokua ndani ya aplikesheni ya M-pesa moja kwa moja" amesema Abdallah
Nakuongeza kwamba "Tunzaa imehudumia watumiaji zaidi ya 25,000 ambao wamejisajili kwenye jukwaa hilo na imewezesha mamia ya wafanyabiashara wanaouza bidhaa zao mbalimbali kupitia jukwaa la Tunzaa.
Aidha amesema kuwa faida zitakazopatikana kupitia Tunzaa ni pamoja na Uwezo wa kupata bidhaa kwa urahisi zaidi,uhuru wa kifedha ulioboreshwa,imani na usalama kwa kizingatia usalama na faragha ya data ya watumiaji ,kuhakikisha utulivu wa akili wakati wa kutumia huduma zilizoingizwa.
Kwa upande wake Meneja Malipo ya Kidigitali na chaneli za mtandaoni kutoka Vodacom M- pesa Josephine Mushi amesema ushirikiano baina yao na Tunzaa ni dhihilisho kua Vodacom imeendeleza kauli mbiyu yake ya pamoja tunaweza ambapo ushirikiano huo utawawezesha wateja wake kununua bidhaa mbalimbali kwa kulipa kidogokidogo mara baada ya kuhifadhi fedha zake Tunzaa.
Comments
Post a Comment