WAZIRI MKUU MAJALIWA AZINDUA KIWANDA CHA KUTENGENEZA VIRUTUBISHI KIKIWA NI CHA PILI BARANI AFRIKA.

Na Moshi said, DSM - 16 Juni 2024.

Waziri Mkuu Kassmu Majaliwa ameitaka Mikoa yenye viwango vikubwa vya upungufu wa damu na udumavu kuanza kutekeleza mpango wa urutubishaji wa chakula kuanzia ngazi ya vijiji 

.

Pia Ameitaka Wizara ya afya na TAMISEMI kuandaa mkakati wa kuelimisha umma kuhusu umuhimu wa kurutubisha vyakula na kula vyakula vyenye virutubisha hususani katika maeneo ya vijijini.

Wito huo ameutoa leo Juni 15/2024 wakati akizindua Kiwanda cha kutengeneza virutubishi (premix blending plant), cha kampuni ya SANKU – PHC Tanzania kilichopo Mikocheni Jijini Dar es salaam ambacho ni cha pili kwa ukubwa Afrika, ambapo Majaliwa amesema kwamba ujio wa kiwanda hicho utasaidia kuboresha afya za wanajamii,kuongeza wigo wa ajila, kupunguza ama kuondoa kabisa gharama za uagizaji virutubishi hivyo nje ya nchi hivyo kupunguza matumizi ya fedha za kigeni.

"Wekeni nguvu kurutubisha vyakula katika maeneo yenye utapiamlo na upungufu wa damu kila mwaka wizara ya afya inatoa takwimu za mikoa yenye changamoto ya lishe duni sasa wekeni nguvu huko ili kupunguza athari zake".

Serikali itaendelea kuwaunga mkono Wazalishaji wa virutubishi SANKU kwa kuwapa kipaumbele kwakuwa ni wazalisha pekee waliopo nchini.pia Serikali itakitangaza kiwanda hicho kwa nchi marafiki na Tanzania kwa manufaa ya pande zote.

Majaliwa pia Amewataka SANKU kutekeleza kwa vitendo adhima ya kutumia malighafi walau aslimia 86 kutoka nchini na endapo watapata changamoto yoyote wawasiliana na watendaji wa Serikali na kupata muafaka wa haraka.

Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa pia Ameitaka wizara ya kilimo na wizara zote zinahusika na uzalisha wa malighafi kuhakikisha wanatoa msukumo kwa wananchi kuongeza jitihada za kulima mazao yanayohitajiks ili kukidhi mahitaji ya kiwanda hicho pamoja na kuongeza tija katika taifa.

Kwa upande wake Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema bado Tanzania inakabiliwa na utapia mlo Ambapo takwimu zinaonesha kwamba kila watoto 100 watatu wanaudumavu huku watoto 100, 30 kati yao wanaukosefu wa vitaminA, na Wanawake 37 kati ya 100 wenye umri wa kuzaa wanakabiliwa na upungufu wa damu.

"Ujio wa kiwanda hiki kitachochea kupunguza kwa kiasa kikubwa tatizo upungufu wa virutubishi kwa watu mbalimbali".

Ameongeza kuwa Serikali imeandaa sera ya afya ya kuongeza virutubishi katika vyakula vinne vinavypendwa zaidi na watanzania Ambavyo ni Unga wa mahindi,mafuta ya kula,chumvi na unga wa ngano hiyo ikiwa ni kukabiliana na utapia mlo.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa SANKU Flelix church amesema kiwanda hicho kina uwezo wa kuzalisha takriban metiki tani 150 za mchanganyiko wa virutubishi kwa mwezi, na kiwanda hicho kitakidhi mahitaji ya wasindikaji unga wote wa Tanzania, Kenya, Ethiopia, Uganda na kwingineko ndani na nje ya katika ukanda wa Afrika ya Mashariki.

"Urutubishaji wa chakula ni mojawapo ya afua za gharama nafuu na zilizothibitishwa na Shirika la Afya Ulimwenguni(WHO) katika kuzuia na kupunguza madhara ya utapiamlo, na uwekezaji katika eneo hili urutubishaji chakula unafaida kubwa Kwenye kila dola 1 (kama TZS 2500) iliyowekezwa, huvuna faida ya dola 27 (TZS 67,500) kwa maana ya kuzuia magonjwa yanayoweza kuepukika, na kuimarika kwa tija ya utendaji kazi kunakoongeza mapato. Hii ndiyo sababu ya Sanku kubuni na kuwekeza katika sualaurutubishaji wa chakula".Amesema Church.

Ameongeza kuwa Kiwanda hicho kinaleta manufaa kadhaa kwa wasindikaji chakula, Serikali, na jamii kwa ujumla,Wasindikaji sasa wataweza kupata virutubishi kirahisi kwa gharama iliyopunguzwa kwa 40% kutoka kwenye kiwango cha sasa cha soko. 

"Napenda kuwafahamisha kuwa asilimia 80 ya malighafi zinazotumika kuchanganya virutubishi, yaani kibebeo ambacho ni ungawa ngano unaohitajika kuchanganya mchanganyiko wa virutubishi utatoka hapa nchini, lakini pia asilimia 70 ya malighafi ya vifungashio vitapatikana kwa wazalishaji wa hapa nchini". 

Serikali itapata mapato kutokana na uendeshaji wa kiwanda, huku jamii ikinufaika na fursa za ajira kwenye mnyororo wa thamani.

Comments