Na.Moshi said - DSM, O4 Julai 2024.
Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi UVCCM Umewataka vijana na Watanzania kwa ujumla kujitokeza kwa wingi katika uzinduzi wa Kampeni maalumu ya vijana itakayo jadili fursa zilizopo kwa vijana katika jamii.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa comrade Joketi Mwegelo amesema kampeni hiyo itazinduliwa siku ya tarehe 06/07/2024 uwanja wa Benjamini William mkapa Jijini Dar es salaam huku ikilenga kujadili fursa zinazoweza kuchangamkiwa na vijana.
Joketi amesema siku hiyo itakuwa fursa kwa vijana kuhamasishwa kujitokeza kujiandikisha katika daftari la kudumu la mpiga kura pamoja na kuwahamasisha vijana kugombea nafasi mbalimbali za uongozi Katika chaguzi zijazo ukiwemo ule wa serikali za mitaa mwaka huu.
Aidha amesema katika kampeni hiyo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Emmanuel Nchimbi na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka ngazi zote Taifa.
Aidha amewasihi vijana na Watanzania wote kujitokeza kwa wingi katika uzinduzi wa kampeni hiyo kwani vijana ndio nguzo muhimu ya maendeleo nchini.
Comments
Post a Comment