Na Moshi said, DSM 9.07.2024
Katibu mkuu Wizara ya Nishati Mhandisi Ferischem Mramba amepongeza kazi zinazofanywa na mamlaka ya kudhibiti wa Nishati na gesi EWURA kwa kazi zinazofanywa na mamlaka hiyo.
Akizungumza wakati alipofanya ziara ya kutembelea Banda la mamlaka hayo kwenye maonyesho ya 48 ya Biashara ya Nje Sabasaba amesema EWURA inawajibu Wa kisheria wa kusimamia Sekta ya Nishati na gesi hivyo imeendelea kufanya vizuri katika kusimamia Sekta hiyo pamoja na kuratibu Shughuli zote zinazofanywa au kusimamiwa na mamlaka hiyo.
Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya Nishati na gesi Tanzania EWURA Dkt.James Andilile amesema wao kama EWURA wameendelea kusimamia ubora na kuhamasisha uwekezaji, ambapo mwezi uliopita waliweza kusaini mkataba na Tanesco wenye lengo la kupimana uwezo wa utendaji kazi, huku pia akigusia maswala mazima ya uwekezaji mkubwa wa Miundombinu uliowekwa na Serikali ikiwemo Mradi mkubwa wa bwawa la kufua Umeme la Mwalimu Julius kambarage Nyerere lililopo Rufiji Mkoani Pwani.
Comments
Post a Comment