WADAU WA KILIMO WAPEWA CHANGAMOTO KUBORESHA MAZAO YAO.

Na Moshi said, Dsm - 16 Julai 2024

Wadau wa mazao ya Nafaka barani Afrika wametakiwa kuendeleza mikakati ya kujinufaisha na mazao hayo, ikiwemo kupata masoko ikiwa sambamba na kuweka mifumo ya sahihi itakayowawezesha kufanya Biashara zenye kuleta tija baina yao.

Akizungumza kwenye kongamano la siku mbili linalofanyika jijini Dar es salaam Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya udhibiti wa nafaka na mazao mchanganyiko, Irene madiji Mola. 

 Mloka amesema mkutano huo unalenga kuzikutanisha nchi zote za Afrika zinazozalisha mazao ya Nafaka ili kutathimini mazao hayo kwenye majukwaa yenye kuweza kuchochea ukuwaji wa kibiashara.

Aidha katika hatua nyingine Mola amesema kwa upande wa Tanzania "tumejipanga katika kufanya mashirikiano na nchi nyingine za Afrika ili kumnufanisha mkulima WA kitanzania ikiwa pamoja Kupata masoko kwenye ya Nje"

Halikadhalika Mloka amezungumzia changamoto zinazowakabiri wakulima na wafanyabiashara wa mazao ya Nafaka ambapo amesema Tanzania kupitia Wizara ya kilimo viwanda na Biashara ili kuweza kuwatatulia changamoto za ikiwemo kuwaunganisha wafanyabiashara ili kuuza Biashara zao wenyewe kwa wenyewe.

Naye  Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Nafaka Africa mashariki amesema wako kama jumuiya wamekutana ili kuangalia uwezekano wa kusaidia wafanyabiashara na wakulima ikiwemo kutatua vikwazo vinavyo wakabiri wadau wote wa Sekta ya mazao ya Nafaka na mikunde. 

Aidha amesema moja ya ajenda kubwa katika mkutano huo ni maswala ya forodha baina ya nchi wanachama pindi wadau waliowekeza kwenye Biashara hizo ikiwemo kuondoka vikwazo mipakani kwenye nchi za Afrika.

Sambamba na hayo wameshauriana juu ya kuongeza thamani ya mazao ya Nafaka ikiwa sambamba na kuhifadhi Usalama wa mazao ya Nafaka na mafuta, ambapo wameomba kupunguza muda WA kupita kwenye mipaka lakini pia kupata soko la uhakika baina ya wadau na wafanyabiashara wa Kutoka nchi za Afrika ya mashariki na kusini mwa Afrika.

Comments