WANANCHI KUIBURUTA TAMISEMI MAHAKAMANI

Na.Moshi said, 27 Agosti 2024.

Wananchi watatu wazalendo Dkt  Ananilea NKYA, Bob Wangwe pamoja na Bubelwa Kaiza wamefungua kesi Mahakama kuu masjala ya Kanda ya  Dar es Salaam, dhidi ya mwanasheria mkuu wa Serikali Kupinga Wizara ya Ofisi ya RaisTawala za mikoa na Serikali za mitaa (TAMISEMI) kusimamia Uchaguzi wa mwaka huu wa Serikali za vijiji, kamati za mitaa na Vitongoji.

Kwa mujibu wa TAARIFA iliyotolewa Leo Agosti 27,2024 na DKT Ananilea NKYA mbele ya Waandishi wa habari jijini Dar es salaam, kuhusu maombi hayo yatasikilizwa jumatano hii, Agosti 28 2024, ambapo awali maombi hayo yalitajwa kwa mara ya Kwanza Agosti 22,  mwaka huu.

Aidha NKYA ambaye pia ni mwenyekiti wa jukwaa la katiba (JUKATA) amewaomba Wananchi kujitokeza kwa wingi kwa lengo la kusikiliza kesi hiyo ambayo itasikilizwa majira ya saa 8 mchana Mahakama kuu masjala ya Kanda ya Dar es salaam.

Kwa upande wake Bob Wangwe amesema kuwa wamefungua shauri Hilo, kwa kuwa wanatambua kwamba raia ndio  mamlaka ya nchi kama inavyothibitishwa na katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 8 (1) (a).

Ameongeza kuwa "SISI raia kwa mamlaka tuliyonayo kwa mujibu na katiba tunapinga, na tunaona ni kinyume cha katiba na Sheria za nchi, iwapo TAMISEMI itasimamia Uchaguzi wa Serikali za vijiji,kamati za mitaa na wenyeviti WA Vitongoji.

Bob Wangwe ambaye pia ni Mkurugenzi mkuu wa JUKATA amesema Uchaguzi ukisimamiwa na mamlaka isiyohusika Kuna hatari Uchaguzi huo kutokuwa na unyoofu, huru na haki na athari zake ni pamoja na kusababisha vijiji mitaa na Vitongoji kuongozwa na watu wasiowaadilifu na wasiowawajibikaji kwa raia hata kufuja michango na Kodi za Wananchi.

Naye Bubelwa Kaiza amesema kuwa hatua hiyo ya kisheria unalenga kulinda haki ya kikatiba ya raia WA Tanzania kushiriki katika mchakato wa kedemokrasia ambao ni nyoofu, na huru na  WA haki.

Amesema kwamba  baada ya kutungwa kwa Sheria ya Tume ya huru ya Taifa ya Uchaguzi mwaka  2024 na kwa mujibu wa katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ibara ya 74 (6) (e), majukumu ya kusimamia Uchaguzi wa Serikali za vijiji, kamati za mitaa wenyeviti WA Vitongoji yako chini ya Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi.

"TAMISEMI Kutaka. Kusimamia Uchaguzi huu ni batili na kinyume cha Sheria,kwa mujibu wa kifungu cha 1 0 (1) (c) cha Sheria Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi pekee yenye Jukumu la kusimamia Uchaguzi wa Serikali za vijiji, kamati za mitaa na wenyeviti wa Vitongoji.

Comments