WANANCHI WATAKIWA KUJITOKEZA KUJIANDIKISHA KATIKA DDAFTARI LA KUDUMU WAPIGA KURA

Na.Moshi said, Kisarawe-Pwani 31.08.2024

Waziri wa Viwanda na Biashara na Mbunge wa Jimbo la kisarawe mkoani Pwani Mh.Suleiman Jafo, amewasihi Wananchi wa Jimbo hilo na watanzania kwa ujumla kujitokeza katika kujiandikisha kwenye maboresho ya Daftari la kudumu la wapiga kura.

Ameitoa kauli hiyo  kwenye kilele cha Tamasha maalum la Sanaa mtaa kwa mtaa lililofanyika jimboni humo.

Waziri  Jafo amesema wakati Taifa likielekea kwenye Uchaguzi wa Serikali za  Vitongoji Vijiji na mit

aa Nchini unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka huu  ni haki ya kila mwananchi kujitokeza na kuhakikisha anajiandikisha kwenye Daftari Hilo ili Kujiandaa  kwa ajili ya kushiriki Uchaguzi huo.

Jafo ambaye pia ametumia fursa hiyo kumpongea Rais  Dkt Samia Suluhu Hassan kwa juhudi zake katika kuwaletea maendeleo Wananchi wa Jimbo hilo  la kisarawe ikiwemo Maji, Elimu, afya pamoja na Nishati ya  Umeme.

Awali akimkaribisha Mgeni rasmi mkuu wa wilaya ya kisarawe Mheshimiwa Petro Magoti amesema kisarawe ya wakati huu imepiga hatua kubwa kimaendeleo chini ya Uongozi wa Serikali ya awamu ya sita chini ya Mheshimiwa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan, hivyo ameitaka jamii kumuunga mkono Mhe. Rais Katika harakati za kuhakikisha anaipeleka mbele nchi katika nyanja mbalimbali za kimaendeleo.

Aidha Magoti ametumia hadhara hiyo kuwaalika wadau mbalimbali kushiriki kwenye TAMASHA kubwa la utalii wa ndani hususani kwenye wilaya ya kisarawe lijulikanalo kama "KULA BATA MSITUNI 2024."

Tamsha ambalo limepangwa kufanyika kuanzia Septemba 22 2024 kwenye msitu wa Kazimzumbwi, Tamsha ambalo linalenga kutangaza vivutio vya utalii vilivyomo ndani ya wilaya hiyo huku mataifa Zaidi ya sita yakitaraji kushiriki Tamasha hilo.

Comments