NISHATI SAFI KUWANUFAISHA WATU MILIONI 300 BARANI AFRIKA - BITEKO

Na Moshi said Dar es salaam, 16 Okt.2024

Naibu Waziri Mkuu  na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko amesema ifikapo mwaka 2030 takribani watu million 300 katika Bara la Afrika wanatarajiwa kufikiwa na umeme ili watu wengi waweze kutumia nishati safi ya kupikia.

Biteko ameyasema hayo  alipokua katika uzinduzi wa mkutano wa 9 wa siku 2 wa soko la Nishati Afrika ulioandaliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika kwa kushirikiana na Wizara ya Nishati unaofanyika jijini Dar es Salaam.

Naibu waziri mkuu huyo amesema kuwa, Benki ya maendeleo ya Afrika imepima kutoka kwa wadau wake wanapata fedha kutoka kwao imeonekana Tanzania imepiga hatua kubwa  na wamefanikiwa, hali iliyopelekea nchi hiyo kuwa shamba darasa kwa wenzao kwenye usimamizi wa Sekta ya nishati.

Amesema kuwa  mkutano huo utakua ni maandalizi ya mkutano wa wakuu wa nchi wa Afrika wanaokwenda kujadili masuala ya nishati kwenye bara la Afrika kwani kuwapata watu 300 sio kazi  rahisi kuishia kwenye ngazi ya Wizara.

Ameongeza kuwa, lengo la mkutano huo ni kwenda kujadili na kufanya tafakuri kubwa kama bara juu ya upatikanaji wa Nishati safi ya kupikia ambapo mfumo wake unachangamoto nyingi kwenye utekelezaji wake.

Halikadhakika , amesema nchi ya Tanzania imepata heshima ambayo haikua kazi rahisi bali kutokana na mahusiano mazuri ya kidiplomasia kati ya nchi hiyo na Benki ya maendeleo ya Afrika AfDB ambapo wamekiri Tanzania imepiga hatua kubwa kwenye masuala ya kisera na usimamizi, uzalishaji na usafirishaji na upelekaji wa umeme Vijijini.

Naye  Makamu Mwenyekiti wa Nishati, mabadiliko ya tabia nchi na ukuaji wa kijani AFDB Dr Kevin kairuki amesema wameamua kufanya kazi kwa pamoja na Tanzania kwa sababu ipo mstari wa mbele katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.

"Tanzania imekua ikitilia manani mambo ya nishati safi ndio sababu tukakaa na wadau kama vile World Benki tukasema hili kongamano lifanyike Tanzania kwani kupata watu million 300 wa kutumia nishati safi ya kupikia sio rahisi" amesema Dr Kairuki.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Eng Felchesmi Mramba amesema mkutano huo wataweza kujadiliana ukuaji wa Nishati, matarajio, namna ya kuipata, uzalishaji na ujumuishaji wa Sekta binafsi kwani ifikapo 2034 wanataka nishati ipatikane kwa unafuu zaidi.







Comments